Philomena Njeri: Ripoti ya Upasuaji Yaonyesha Hakuwa Mjamzito

July 2024 ยท 2 minute read

Ripoti ya upasuaji wa mwili wa Philomena Njeri aliyeuawa na Jonathan Mukundi imeonyesha hakuwa mjamzito kama ilivyodaiwa.

Ripoti zilikuwa zimeibuka kuwa Njeri aliuawa baada ya Mukundi kufikiwa na taarifa kwamba alikuwa na ujauzito.

Mukundi alichomwa roho kuwa mpenziwe alikuwa amebeba mimba ya jamaa aliyeshuku alikuwa mpenzi wake wa kando.

Kulingana na ripoti ya upasuaji wa maiti, Njeri alifariki dunia baada ya kupigwa risasi nne; mbili tumboni na mbili kwenye kichwa.

Mpasuaji wa serikali Johanes Oduor alisema Mukundi alijipiga risasi ya kichwa iliyoingia kupitia upande wa kulia na kutokea kushoto.

Miili ya waili hao ilipatikana Jumanne Agosti 3 ikiwa katika chumba chao kilichokuwa kimefungwa upande wa ndani.

Pia soma

Magazeti Ijumaa Julai 6: DP Ruto Asema Atachomoka Kutoka Serikali Wakati Ukifika

Rafiki wake Mukundi ndiye alipiga ripoti baada ya kumpigia simu lakini hakuwa akijibu na polisi walipofika kwake wakalazimika kuvunja mlango.

Kwa mujibu wa duru za kuaminika ambazo zimezungumza na meza ya TUKO.co.ke, wawili hao walikuwa na mzozo wa kifamilia.

Njeri alirejea nyumbani kwa Mukundi Jumatatu Agosti baada ya kipindi cha kutengana kutokana na tofauti.

Jumatattu hiyo, wawlikuwa wamekutana kwenye mkahawa mmoja kujaribu kumaliza tofauti zao lakini hawakuelewana.

Saa chache baadaye, Mukundi alimuita Njeri akimwarifu alikuwa amepata ajali na alihitaji usaidizi wake ili ampeleke hospitali.

Habari Nyingine: Ruto 'Ang'olewa Kucha' na Habari Zingine Zilizotikisa Anga Wiki Hii

Polisi wanaamini hiyo ilikuwa tu njama ya Mukundi kumhadaa afike nyumbani ili ammalize na kisha kujiua.

Wanaoijua familia hiyo wameitaja na iliyokuwa na mifuko mizito lakini waliteswa na ukosefu wa mtoto licha ya ndoa ya miaka 10.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.

Pia soma

Jonathan Mukundi: Taarifa Zaidi Zaibuka Kuhusu Mauaji ya Philomena Njeri Kiambu

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdkZ352hY9mp6GhnKS6prrAZqWjnaKeerO1z6iromWplnq2vMCsrJqimWLGorvNspysoJFitaK31LCYZqWalrq7tdOoZaGsnaE%3D